Exim Bank
 • comoros
 • djibouti
 • uganda
Search

wakala

EXIM Bank Wakala

Exim Bank Wakala

Pata huduma za Kibenki kupitia Wakala wa Benki ya Exim popote karibu yako!

1. Namna ya kumtambua Wakala wa Benki ya Exim

 • Mawakala wote wa Exim bank wanakuwa na bango au kiashiria chenye alama na rangi tambulishi za Exim bank.

2. Huduma zinazotolewa na Wakala wa benki ya Exim ni pamoja na zifuatazo;

 • Kuweka fedha kwenye akaunti ya benki ya Exim (Cash Deposit)
 • Kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya benki ya Exim (Cash withdraw)
 • Kuhamisha Fedha kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine ya benk ya Exim bank (Fund Transfers)
 • Kuuliza Salio la akaunti yako (Balance Enquiry)
 • Taarifa Fupi ya akaunti yako (Mini-Statement)

3. Huduma nyingne unazoweza kupata kupitia Wakala wa Benki ya Exim:

 • Kulipia manunuzi ya bidhaa (Payments of Goods)
 • Kulipia bili/ankara za huduma mbalimbali (Utility Bill Payments)
 • Kulipia malipo mbalimbali ya Serikali (GePG Payments)  
 • Kulipa kodi mbalimbali za TRA (TRA TAX Payments)

4. Faida za Wakala wa Benki ya Exim

 • Inakupatia huduma za kibenki karibu na mahali ulipo
 • Inakupatia huduma za kibenki kwa Gharama nafuu
 • Inaokoa muda na gharama za kufuata huduma Tawini au kwenye ATM
 • Inakuwezesha kufanya huduma mbalimbali za kifedha ukiwa sehemu moja tu
 • Inakusaidia kuepuka Foleni na kukupatia huduma katika mazingira marafiki

5. Jinsi ya kuhakikisha kua muamala wako umefanyika sawa sawa.

 • Kila baada ya muamala kukamilika ,utapokea Ujumbe mfupi wa meseji wa uthibitisho wa muamala kutoka benki ya Exim.
 • Risiti kutoka kwa Wakala wa Benki ya Exim inayothibitisha kufanyika na kukamilika kwa muamala.

6. Usalama wa huduma kutoka kwa Wakala wa Benki ya Exim

 • Kufanya muamala kupitia kwa Wakala wa Benki ya Exim kuna usalama wa hali ya juu kutokana na sababu zifuatazo;
 • Mawakala wa Benki ya Exim wanafundishwa kwa umakini na kusimamiwa kila mara kwa utaratibu unaofaa na vilevile wamepewa uwezo wa kutambua na kuzuia aina yoyote ya utapeli  katika mazingira yao ya kazi
 • Mfumo wa uwakala umeunganishwa moja kwa moja na ule wa benki hivyo kila muamala unapofanyika,moja kwa moja unakwenda benki muda huo huo
 • Kila muamala ufanyikapo kupitia Mawakala wa Benki ya Exim, mteja hutumiwa ujumbe mfupi  wa meseji wenye maelezo ya muamala huo hivyo kufanya huduma hii kuwa salama zaidi

Angalizo: Si lazima mteja kuwa na kadi yake ya benki ili kupata huduma kupitia mawakala wa benki ya Exim.

To know more, get in touch!