Exim Bank
  • comoros
  • djibouti
  • uganda
Search

Diaspora Banking

Diaspora Banking

Bidhaa ya kibenki iliyotengenezwa kuhudumia Watanzania wanaoishi nje ya nchi, ili kuzifikia huduma na bidhaa za Benki ya Exim kama vile, Kununua/kuhamisha mikopo, amana, huduma za mikopo ya nyumba, ununuzi wa nyumba na fursa nyingine za uwekezaji kulingana na matakwa ya wateja. Ukiwa na Serengeti Diaspora akaunti, utaweza kufungua akaunti kwa urahisi na kufanya miamala kwa usalama zaidi, chini ya uangalizi wa meneja uhusiano atakayehakikisha unahudumiwa vizuri.

Akaunti ya Serengeti Diaspora itakupatia;

  • Meneja uhusiano kupitia bidhaa yetu ya Preferred banking.
  • Kufanya miamala kwa urahisi na salama zaidi kupitia akaunti inayoweza kuendeshwa mtandaoni.
  • Huduma za bima ya Maisha kwa ajili ya diaspora na familia yake mpaka Tsh 31,450,000.
  • Kiwango kizuri cha riba ya amana, na ada/makato nafuu kwa akaunti ya miamala (Current Account) na hakuna makato ya kila mwezi kwenye akaunti za amana (Savings Account).
  • Fursa za kuwekeza ndani ya Tanzania.

Mahitaji ya kufungua Akaunti:

Tanzanian Citizen Diaspora

  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Pasipoti ya Tanzania TZ.
  • Picha mbili za passport.
  • Kimojawapo kati ya hivi (Driving License, Student ID, Voters ID, Certified copy of the resident, Working permit/Work/Employment ID)
  • Uthibitisho wa anuani ya makazi- Bili ya matumizi ya nyumbani yenye jina la mwenye akaunti.

Non-Citizen Tanzanian Diaspora

  • Kitambulisho cha Taifa au Pasipoti ya nchi aliyopo.
  • Picha mbili za passport.
  • Vitatu kati ya hivi (Driving License, Student ID, Voters ID, Certified copy of the resident,Working permit/Work/Employment ID).
  • Uthibitisho wa anuani ya makazi- Bili ya matumizi ya nyumbani yenye jina la mwenye akaunti.

Ukiwa na Serengeti Diaspora Banking, utaweza kufurahia aina za akaunti zifuatazo;

  1. Serengeti Diaspora Current Account

    Akaunti binafsi iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya wateja ambao wameajiriwa, wamejiajiri, au wanafunzi ambao wanahitaji kutuma pesa kwa ndugu jamaa na marafiki kwa urahisi zaidi. Lakini pia, akaunti hii ni kwa ajili ya wateja walio nje ya nchi wanaomiliki biashara zilizosajiliwa na kuendeshwa ndani ya Tanzania.

    Sifa na faida za Akaunti hii

    • Inaweza kufunguliwa na kuendeshwa kwa TSH/USD/EUR/GBP.
    • Kiwango cha chini cha kufungua akaunti ni TSH 100,000 au USD/EUR/GBP 100.
    • Unaweza kutumia Exim MasterCard kufanyia malipo popote ulipo duniani.
    • Ufikiaji wa huduma zetu za kibenki mtandaoni utakaokupa urahisi wa kuendesha akaunti yako na kufanya miamala.
  2. Serengeti Diaspora Savings Account

    Akaunti ya akiba inayowawezesha wateja wetu kuweka akiba nyumbani huku wakiwa nje ya nchi.

    Sifa na faida za Akaunti hii

    • Inaweza kufunguliwa na kuendeshwa kwa TSH/USD/EUR/GBP.
    • Kiwango cha chini cha kufungua akaunti ni TSH 100,000 au USD/EUR/GBP 100.
    • Ufikiaji wa huduma zetu za kibenki mtandaoni utakaokupa urahisi wa kuendesha akaunti yako.
    • Riba ya amana mpaka asilimia 5 kwa akaunti za Tsh na asilimia moja kwa akaunti za TZS/USD/EUR/GBP.
    • Hakuna ada ya kuendesha akaunti.
  3. Serengeti Diaspora Mortgage Financing

    Pata suluhisho la mkopo wa nyumba kupitia bidhaa ya Mikopo ya Exim Nyumba yangu.

    1. Mkopo wa kununua Nyumba
      • Bidhaa hii inawawezesha wateja wetu kufurahia fursa ya kununua nyumba ya makazi binafsi au ya kupangisha.
      • Uhamisho wa haki za umiliki unafanywa kabla ya pesa kuhamishwa kwa muuzaji, na hati itakayoletwa benki lazima iwe katika jina la mteja.
    2. Mkopo wa Nyumba
      • Huduma hii inatolewa kwa mteja ambaye anataka kupata pesa ya nyongeza kununua nyumba,na mteja ambaye ameshawekeza pesa binafsi kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi anayetaka nyongeza ya pesa katika kukamilisha ujenzi.
      • Uwiano wa mkopo kwa thamani iliyokadiriwa ya mali ni asilimia 80.
    3. Kuhamisha/Kununua mkopo wa nyumba
      • Huduma hii inatolewa kwa mteja ambaye anataka kupata pesa ya nyongeza kununua nyumba,na mteja ambaye ameshawekeza pesa binafsi kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi anayetaka nyongeza ya pesa katika kukamilisha ujenzi.
      • Uwiano wa mkopo kwa thamani iliyokadiriwa ya mali ni asilimia 80.

      Sifa na faida za bidhaa hii;

      • Kiwango cha chini cha mkopo ni TSH 30,000,000.
      • Kiwango cha juu cha mkopo ni TSH 500,000,000.
      • Muda wa marejesho ni mpaka miezi 180.
      • Mikopo inashughulikiwa na kutolewa kwa muda mfupi.
      • Kununua/kuhamisha mkopo kwa vigezo na masharti yenye manufaa.
      • Hakuna Ada zilizofichwa.

      Mahitaji ya kufungua Akaunti;

      • Muombaji awe na umri kati ya miaka 21 - 58.
      • Kama kiasi cha kipato hakitoshi, inaruhusiwa kuunganisha kipato cha mke/mme kama akiridhia.
      • Bima ya mali na Maisha kwa muombaji ni lazima.
      • Tathmini ya mali lazima ifanywe na wafanya tathmini waliothibitishwa na Exim Bank.
      • Mkopo unatolewa kwa wafanyakazi walioajiriwa na wafanyabiashara.
  4. Cash Cover Loans

    Hii ni mikopo ya muda na overdraft inayoruhusiwa na Benki kwa wenye akaunti za amana maalum. Unaweza kupata mikopo ya mpaka asilimia 90 ya kiwango kilichopo kwenye akaunti yako ya amana maalum.

    Sifa na faida za bidhaa hii;

    • Kiwango cha chini cha mkopo ni TSH 1,000,000.
    • Kiwango cha juu cha mkopo ni asilimia 90 ya kiwango kilichopo kwenye akaunti, mpaka miezi 60.
    • Marejesho ni kwa awamu sawa za kila mwezi kwa mkopo wa muda, na malipo ya riba yaliyokubaliwa kwa kipindi cha mkopo.
    • Mikopo inashughulikiwa na kutolewa kwa muda mfupi.
    • Kununua/kuhamisha mkopo kwa vigezo na masharti yenye manufaa.
    • Hakuna Ada zilizofichwa.

    Mahitaji;

    • Uwe na akaunti ya amana maalum Exim Bank.
    • Barua ya maombi iliyotimia na picha mbili za passport size zenye rangi.
    • Nakala ya kitambulisho chako (Passport,kitambulisho cha mpiga kura, NIDA, Leseni ya udereva, kitambulisho cha Zanzibar).
  5. Suluhisho lingine la uwekezaji linalowawezesha Diaspora kufurahia amana za kudumu
    • Weka akiba kwa ajili ya malengo ya muda mfupi na mrefu huku ukipata faida kupitia viwango vyetu shindani vya riba.
    • Weka akiba kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja mpaka miaka minne. Nafuu ni kwamba, unachagua mwenyewe muda wa kuweka akiba kulingana na malengo yako. Muda ukiwa mrefu ,riba itakuwa nyingi.

    Sifa na faida za bidhaa hii;

    • Akaunti ya amana maalum inaweza kufungliwa kwa TSH/USD/EUR/GBP.
    • Kwa kiwango cha chini cha TSH 1,000,000 au USD/EUR/GBP 100, unaweza kuchagua kufungua akaunti ya amana maalum zaidi ya moja, au pesa zako zote ziwe kwenye akaunti moja.
    • Mifumo wetu imara ya ulinzi itahakikisha pesa zako zipo salama masaa 24 kila siku.
  6. Haba na Haba Plus Account

    Akaunti ya Haba na Haba ni maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wanaohitaji kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya matumizi ya baadae. Bidhaa hii imelenga kuhamasisha uwekaji wa akiba ya pesa. Akaunti hii ya Haba na Haba Plus ni mahsusi kwa ajili ya wateja wenye kipato cha juu wanaopokea viwango vya juu vya riba.

    Sifa na faida za bidhaa hii;

    • Kiwango cha riba mpaka asilimia 7 kwa mwaka. (inahesabiwa kwa akiba ya kila siku).
    • Kiwango cha chini cha amana maalumu cha TSH 10,000,000.
    • Hakuna ada za kuendeshea akaunti kila mwezi.
    • Huduma iliyotukuka katika matawi yetu yote.
    • Huduma zinazoendana na thamani ya pesa yako kutoka kwa mameneja uhusiano wetu waliobobea.
  7. Nyota Savings Account

    Watoto ndio taifa la kesho na inatupasa kutengeneza msingi imara kwa ajili ya hiyo kesho yao, hiyo ndio itakuwa zawadi yenye tija tunayoweza kuwapa. Akaunti ya akiba ya Nyota ina mpango mahsusi na dhabiti unaolenga kumpa mtoto wako kesho yenye matumaini, na ambayo itatimiza ndoto zake.

    Sifa na faida za bidhaa hii;

    • Akiba ya kila mwezi: Weka kiasi kidogo cha pesa au amana maalum ndogo kila mwezi kwenye akaunti yenye jina la mtoto wako *(Kiwango cha chini ni 10,000).
    • Akiba ya muda maalum: Fungua akaunti ya amana maalum uweke akiba kwa muda wa mwaka mmoja kwa TSH au USD, ufurahie riba shindani.
    • Faida za muda kumalizika: Jumla ya akiba uliyoweka na Riba yake.
    • Zawadi: Akaunti ya amana maalum inaweza kuzawadiwakwa ndugu wa mtoto.

ALLIANCE LIFE ASSURANCE LIMITED GROUP FUNERAL ASSURANCE (GFU) BENEFITS DIASPORA

Mwenye Bima VIFURUSHI VYA BIMA[TSH]
Chaguo la kwanza Chaguo la pili Chaguo la tatu
Mwanachama 7,000,000 10,500,000 11,750,000
Mwenza 5,000,000 8,200,000 9,500,000
Watoto (mpaka watoto wanne) 4,500,000 4,700,000 5,500,000
Faida ya rejesho kwa mwanachama tu 4,500,000 4,700,000 4,700,000
Jumla ya faida 21,000,000 28,100,000 31,450,000
Malipo ya kila mwaka kwa familia moja 165,000 230,000 270,000
Mwenye Bima VIFURUSHI VYA BIMA[USD]
Chaguo la kwanza Chaguo la pili Chaguo la tatu
Mwanachama $ 3,000 $ 4,500 $ 5,000
Mwenza $ 2,000 $ 3,500 $ 4,000
Watoto (mpaka watoto wanne) $ 2,000 $ 2,000 $ 2,500
Faida ya rejesho kwa mwanachama tu $ 2,000 $ 2,000 $ 2,000
Jumla ya faida $ 9,000 $ 12,000 $ 13,500
Malipo ya kila mwaka kwa familia moja $ 70 $ 95 $ 115

Badilisha lugha - English

To know more, get in touch!
1st
Bank from Tanzania in Djibouti