Exim Bank
  • comoros
  • djibouti
  • uganda
Search

Insurance

Exim Bank Insurance

Insurance

Pamoja Hadi Mwisho:

Pamoja Hadi Mwisho ni Bima ya maisha kwa vikundi rasmi au visivyo rasmi yenye lengo la kusadia vikundi na wanavikundi dhidi ya majanga yatokanayo na Vifo, Ulemavu wa Kudumu na Elimu kwa Watoto wanaoachwa pindi mwanachama anapo fariki. Bima hii ya Pamoja Hadi Mwisho imeletwa kwako kwa lengo la kuhakikisha huwaachwi nyuma linapokuja suala la kujilinda wewe na familia yako uipendayo.

Faida za Bima ya Pamoja Hadi Mwisho:

  • Hakuna muda wa kusubiri (Waiting Period).
  • Kumlinda mwanachama, mweza, wazazi, wakwe na watoto (Hadi 4) kwenye janga la kifo.
  • Kumlinda mwanachama pale anapopata ulemavu wa kudumu unaotokana na Ajali.
  • Uhakika wa watoto (Hadi 4) kuendelea na shule katika mwaka husika endapo kifo cha mwanachama kitatoke.

Jinsi ya Kujiunga

  • Bima hii ni ya vikundi pekee vinanvyoanzia watu 3 na kuendelea.
  • Wanachama watajaza fomu ya Bima ambazo wataweka taarifa zao husika.
  • Kiongozi wa kikundi atajaza fomu ya mapendekezo kwa niaba ya kikundi.
  • Ada ya Bima ilipwe yote mara moja (Mwaka mzima).
  • Umri wa mtoto ni kuanzia miaka (0-21).
  • Umri wa mwanachama ni kuanzia miaka (18-75).

MAFAO YA BIMA YA PAMOJA HADI MWISHO

MAELEZO YA HUDUMA

IMARA

HAKIKA

SALAMA

Kifo cha mwanakikundi

TZS 3,500,000

TZS 4,500,000

TZS 6,000,000

Ulemavu wa kudumu wa mwanakikundi

TZS 3,500,000

TZS 4,500,000

TZS 6,000,000

Kifo cha Mke/Mume

TZS 2,000,000

TZS 3,500,000

TZS 5,000,000

Kifo cha mtoto (Hadi 4)

TZS 1,000,000

TZS 1,000,000

TZS 1,500,000

Mafao ya elimu kwa watoto (Hadi wa 4) baada ya kifo cha mwanakindi

TZS 1,000,000

TZS 1,000,000

TZS 1,000,000

Kifo cha Mzazi

TZS 500,000

TZS 500,000

TZS 500,000

Kifo cha mkwe

TZS 500,000

TZS 500,000

TZS 500,000

Ada ya mwezi

TZS 4,450

TZS 5,250

TZS 6,250

Ada ya mwaka

TZS 53,400

TZS 63,000

TZS 75,000

To know more, get in touch!