Exim Bank
  • comoros
  • djibouti
  • uganda
Search

Mastercard ChanjaKijanja

Benki ya Exim yazindua kampeni ya Chanja Kijanja kwa wateja wake wanao miliki kadi za Mastercard.

ChanjaKijanja na Exim Bank Mastercard

Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni ya uhamasishaji ikilenga kuwashawishi zaidi wateja wa benki hiyo kutumia kadi za Mastercard ambapo pamoja na mambo mengine itatoa zawadi mbali mbali kwa wateja hao.

Uzinduzi wakampeni hiyo mpya iliyopewa jina la 'Chanja Kijanja na Exim Mastercard' unalenga hiyo kutoa fursa ya kipekee kwa wateja wa benki hiyo kufurahia huduma zinazo kwenda sambamba na mfumo wa maisha yao kupitia benki hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo, kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi za benki hiyo katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.

"Kwa upande wetu Benki ya Exim, wateja wanao tumia kadi zetu wamekuwa wakifurahia urahisi wanapofanya manunuzi au malipo kwenye ya mahitaji muhimu kwenye maduka (Shopping), ununuzi wa bidhaa kimataifa kupitia mtandaoni, malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli na shughuli za kitalii. '' Alisema.

"Kwasasa, si tu kwamba wateja wetu wanafurahia urahisi mkubwa unaotokana na matumizi ya kadi za benki ya Exim, bali pia wanapata fursa ya kushinda zawadi nzuri kupitia kampeni hii. Kutakuwa na zawadi za kila wiki na kila mwezi wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya mihamala yao kupitia kadi ya Exim Mastercard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kila muhamala unaongeza nafasi moja ya kushinda,'' aliongeza.

Alibainisha kuwa wakati wa kampeni hiyo, jumla ya washindi 10 wa kila wiki watapata zawadi za vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi  50,000 huku kila mwezi washindi watano (5) watazawadiwa simujanja (smartphones).

Akizungumzia zawadi kubwa kwenye kampeni hiyo Bw. Lyimo alisema washindi pamoja na wenza wao watatunukiwa zawadi ya kusafiri wakiwa wamegharamiwa gharama zote ikiwemo Visa, Tiketi ya Ndege pamoja na pesa za matumizi.

"Mshindi wa kwanza ataenda Dubai, mshindi wa pili ataenda Cape Town, Afrika Kusini na wa tatu ataenda visiwa vya Zanzibar.'' alitaja.

Kwa mujibuwa Mr. Lyimo, Kampeni hiyo itaanza katikati ya mwezi Februari hadi mwisho wamwezi Aprili 2020 na ipo wazi kwa wateja wote wanao miliki kadi za Exim MasterCard, pamoja na wateja wote ambao wameomba au wataomba kadi mpya katika kipindi cha kampeni.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bwana Stanley Kafu, alielezea kufurahishwa kwake na uzinduzi wa kampeni hiyo akisema, "Tumefurahishwa sana na ujio wa kampeni ya Chanja Kijanja. Kuongeza ubora wa huduma za kibenki kwa wateja wetu huku tukifanya matumizi yao kuwa na faida kwao ndio falsafa ya kiutendaji hapa benki ya Exim'' alisema.

"Benkiya Exim itaendelea kutoa ofa na zawadi za kipekee kwa wateja wake, kama ishara ya kuthamini imani na uaminifu wao kwetu. Ni furaha kwetu kuona tunagusa hisia za wateja wetu kupitia kampeni hii. Kutumia kadi ya Exim MasterCard ni njia ya haraka, rahisi na salama ya kufanya ununuzi wa kila siku…hivyo basi wewe ChanjaKijanja na Exim Bank Mastercard,'' alisisitiza.

Dar es Salaam; Februari 17, 2020.
To know more, get in touch!