Exim Bank
  • comoros
  • djibouti
  • uganda
Search

Deposit Utokelezee na Exim


Benki ya Exim yazindua kampeni ya ‘Deposit Utokelezee na Exim’

Benki ya Exim yazindua kampeni ya Deposit Utokelezee na Exim

Dar es Salaam: Novemba 19, 2018: Benki ya Exim Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo inawawezesha wateja wa benki hiyo kupata viwango vya riba vya kuvutia hadi asilimia 10.5 ikiwa watafungua akaunti ya amana maalum (fixed deposit) au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi kisichopungua Sh 50m/- kabla ya Desemba 31 mwaka huu..

"Kampeni hii inalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania. Kwa kuzingatia viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi 10.5% kwenye amana zao, " Alisema Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda wakati hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.

Bi Kaganda aliongeza, "kama benki, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wateja wetu, ili kuhakikisha wanakua na ustawi mzuri sasa na hata baadae. Kupitia akaunti zetu za muda maalum (Fixed deposit) mteja anaweza kuongeza kiasi kikubwa cha pesa huku akiwa na uhuru wa kuchagua aina ya muda anaotaka. Tunaamini kwamba kesho yako bora inaanza leo.’’

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997, Benki ya Exim imefanikiwa kujitanua maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo kwasasa ina matawi yake kwenye mikoa 13 nchini ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara. Pia matawi yake yapo kwenye nchi za Comoros, Djibouti na Uganda.

To know more, get in touch!